Psalms 107:23-26


23 aWengine walisafiri baharini kwa meli,
walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.
24 bWaliziona kazi za Bwana,
matendo yake ya ajabu kilindini.
25 cKwa maana alisema na kuamsha tufani
iliyoinua mawimbi juu.
26 dYakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini,
katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.
Copyright information for SwhNEN